Waziri wa Vijana na Michezo anakagua maandalizi ya Taasisi ya GENU kwenye kituo cha maendeleo ya vijana kiko Aljazira

Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo akikagua maandalizi ya mwisho ili kuandaa taasisi ya GENU kwenye kituo cha maendeleo ya vijana kilichoko aljazira, ndani ya ushirikiano kati ya wizara na shirika la umoja wa matiafa la kuwahudumia watoto (UNICEF), kwa lengo la kukuza ujuzi wa vijana, kuunga mkono elimu, ujasirimali na ajira kwa vijana.
Aliambatanwa na Bw. Khader Kamal, Kaimu mwakilishi mkazi wa UNICEF na Dkt. Ghada Mkadi, Mkuu wa mipango ya vijana wa UNICEF, ambapo wahudhuria walionesha hatua zilizotimizwa za maandalizi ya taasisi, zaidi ya mipango ya mafunzo yaliyoamuliwa kuzinduliwa hivi karibuni.
Wakati wa ziara hiyo, Dkt. Ashraf Sobhy alisisitiza kwamba taasisi ya GENU ni mfano Mkuu wa kusaidia vijana vya Misri, akivuta kuwa ni miongoni mwa mkakati wa wizara kuwezesha vijana na kuwaandaa kujiunga soko la ajira.
Akiongeza kuwa hatua ya kwanza ya mpango inalenga kufunza na kujenga uwezo wa vijana milioni 13, na ajira kwa vijana milioni moja, na hivyo kupitia kukuza ujuzi wao kwenye elimu, ujasirimali na kusaidia ushiriki wao wa kijamii.
Waziri alibainisha kushukuru kwake kwa jukumu muhimu linalofanywa na UNICEF la kusaidia na kutekeleza mpango wa kitaifa " Shabaab balad", akisisitiza umuhimu wa kukuza ushirikiano wa pamoja kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu yanayonufaisha vijana wa Misri. Kwa upande wake, Bw. Khader kamal alithibitisha kuwa UNICEF inathamini ushirikiano wake pamoja na serikali ya misri na wizara ya vijana na michezo, na inasaidia uwekezaji wa kukuza ujuzi wa vijana, kutosheleza fursa za kujifunza na ajira zinazowawezesha kutimiza ndoto zao na kuchangia katika jamii zao. Akiashiria kuwa taasisi inaamuliwa kufunguliwa mnamo robo ya kwanza ya mwaka ujao, na hiyo ni hatua muhimu ya kukuza uwezo wa vijana.
Na Dkt. Ghada Makadi alisisitiza kuwa UNICEF itaendelea kusaidia juhudi za kitaifa zinazolenga vijana, akivuta kuwa taasisi ya "GENU" itachangia kikubwa kuandaa kizazi mwenye uwezo wa kukabiliana na changamoto za siku za usoni na kufikia maendeleo endelevu.
Kinachostahiki kusemwa ni kuwa taasisi ya "GENU" kinakuja ndani ya mpango wa kimataifa "generation unlimited" (Shabaab balad), unaolenga kuongeza ujuzi,fursa za kujifunza, ajira na ujasiriamali kwa vijana bilioni 1.8 duniani kote. Na Misiri inazingatiwa ni nchi ya kwanza kwenye eneo linalozindua toleo la kitaifa ya mpango huo chini ya jina la "Shabaab balad", inayolenga kuwezesha uhamisho wa vijana kutoka awamu ya kujifunza kwenda awamu ya kazi na kufikia kujitosheleza.
Ushirikiano huo unakuja ndani ya muono wa Misiri wa 2030 unaolenga kuimarisha ushirikiano kati ya mamlaka ya serikali na taasisi ya kimataifa, na kutosheleza mazingira ya kuhamasika ya kukuza uwezo wa vijana na kuwawezesha kwenye ngazi zote.