Wizara ya Vijana na Michezo: Toleo la pili la Shindano la “Mwanzo wa Ndoto” ina Uangalifu mwema wa Mke wa Rais wa Jamhuri.


Dkt. Ashraf Sobhy:


Uangalifu wa Mke wa Rais wa shindano la "Mwanzo wa Ndoto" kwa mwaka wa pili ni mwendelezo wa thamani halisi iliyoongezwa inayowakilishwa na shindano hilo. 


Shindano la "Mwanzo wa Ndoto" ni kama sehemu ya juhudi za Wizara kuwawezesha vijana na kuongeza michango yao.


Wizara ya Vijana na Michezo ilitangaza kumdhamini Mke wa Rais wa Jamhuri kwa ajili ya toleo la pili la shindano la  mwanzo wa ndoto” ambalo linatekelezwa na Wizara kupitia Uongozi Mkuu wa Maendeleo ya Vijana (Utawala Mkuu wa Chuo Kikuu wa Programu na Shughuli) kwa kikundi cha umri (miaka 18-40).


Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alithibitisha kwamba udhamini wa Mke wa Rais wa “Mwanzo wa ndoto” kwa mwaka wa pili ni mwendelezo wa thamani halisi inayowakilishwa na shindano hilo, na unaonyesha kuhishima na kuendelea nchini Misri, kwa mawazo ya vijana na ushiriki wao katika suala la kuimarisha utambulisho wa taifa la Misri na kuondokana na matatizo na changamoto zinazoikabili, na kufanya kazi ili kuweka matarajio ya vijana mstari wa mbele wa ajenda ya kitaifa kama msingi thabiti wa kuzindua na pamoja na mihimili ya Jamhuri mpya ya Misri.


Waziri huyo alisema kuwa shindano la "Mwanzo wa Ndoto" ni sehemu ya juhudi zinazotolewa na Wizara ya Vijana na Michezo kuwawezesha vijana, kuongeza michango yao, na kunufaika nao katika ngazi zote za kitaifa kwa kupitisha mipango mingi ya vijana na kubadilisha maoni na mawazo ya vijana kuwa Programu na miradi inayochangia katika kujenga taifa.


Shindano hilo lilikuwa miongoni mwa malengo ya jumla ya kimkakati ya serikali, ambayo inafanya kazi ya kuuunda mtu wa Misri na kuunganisha utambulisho wake kwa kufanya mifumo ya kitaasisi ambayo inawahimiza vijana kuwa wabunifu ili kufikia uongozi kwa Misri katika nyanja zote.


Shindano la "Mwanzo wa Ndoto" ndilo shindano kubwa zaidi la mawazo na wakuu  wa mipango katika ngazi ya Jamhuri ambalo linalenga kufikia asilimia kubwa zaidi ya ushiriki wa vijana katika ujenzi wa jamii, kuboresha mawazo yanayohusiana na kazi za kitaifa na mipango ya jamii, kufundisha na kufuzu kwa vijana na kuinua viwango vya ufanisi na tija, pia inalenga kujumuisha kanuni, maadili na tabia nzuri kupitia kazi pamoja na kuunganisha kwa ufanisi kati ya mipango mbalimbali na malengo ya Dira ya 2030 kwa njia ambayo huongeza imani ya vijana katika mfumo jumuishi wa kitaifa, kufikia mifano chanya na kuunganisha kanuni ya malipo inayohusishwa na ustadi na tija.