Waziri wa Vijana na Michezo afikia mkoani Matruh kukagua majengo ya vijana na michezo

Alhamisi, Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alifikia katika makao makuu ya serikali ya mkoa wa Matruh, na kupokelewa na Meya Khaled Shoaib wa Matruh, kabla ya kuanza mpango wake wa ziara katika mkoa huo, ambayo inajumuisha majengo mbalimbali ya vijana na michezo katika mkoa wa Matruh.
Ziara hiyo inakuja katika mfumo wa ziara za ukaguzi za Waziri wa Vijana na Michezo katika mikoa ya nchi, kufuatilia utekelezaji wa kazi katika majengo ya vijana na michezo, na kujua kwa maendeleo ya hivi punde kuhusu uboreshaji na kuongeza ufanisi wake, na kufanya kazi ili kuimarisha jukumu lake la kijamii, na kuongeza manufaa ya huduma zinazotolewa na majengo haya kwa vijana katika umri mbalimbali.
Waziri wa Vijana na Michezo alisisitiza kuwa mkoa wa Matruh ni lango la Misri Magharibi na ngome yake imara, akiashiria kuwa wizara ina nia kubwa katika kuboresha majengo ya vijana na michezo ili kuwahudumia watu wengi zaidi katika mkoa wa Matruh, katika mfumo wa maono ya Misri 2030, na katika mfumo wa umakini wa uongozi wa kisiasa kwa mikoa ya mpakani.
Mpango wa ziara wa Waziri wa Vijana na Michezo katika mkoa wa Matruh inajumuisha ukaguzi wa kambi ya Chama cha Al-Kashafa Albahria (Waskaut wa Baharini) karibu na kituo cha huduma za dharura cha pwani, na kuandaa mkutano wazi katika Maktaba ya Misri ya Umma na vijana wa mkoa (wanachama wa baraza la wabunge, wakuu wa vilabu na vituo vya vijana, wanachama wa mfano wa Bunge la Seneti na Bunge la Vijana na Vizazi vijavyo, vijana, wahitimu wa Chuo cha Nasser, wanachama wa vilabu vya kujitolea, na klabu ya uongozi wa vijana).
Mpango huo pia unajumuisha ufunguzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa watu watano katika Kituo cha Vijana cha Matruh, na kuhudhuria mechi ya mpira wa miguu katika michuano ya Olimpiki ya mikoa ya mpakani, na kukagua shughuli za uskaut na shughuli za wavulana wa uskatu katika Kituo cha Vijana cha Matruh, na kukagua maonesho ya bidhaa za vilabu vya wasichana na wanawake, na maonyesho ya miradi iliyoshinda katika programu ya”Natashark” (Tunashirikiana) kwa ajili ya miradi ya jamii, na maonyesho ya sanaa ya plastiki, na klabu ya kitamaduni, na vile vile mechi ya mpira wa mikono katika michuano ya Olimpiki ya mikoa ya mpakani huko Matruh, na maonyesho ya mradi wa kitaifa wa bingwa wa Olimpiki katika mchezo wa judo, pamoja na mradi wa kitaifa wa wasichana elfu moja ndoto elfu moja, na onyesho la michezo la timu ya chezo cha kimwili.
Pia inajumuisha mpango wa ziara wa ukaguzi wa shughuli za mpango ya Yala kamp katika mji wa Siwa, na ushiriki katika tamasha la kutembea, na ukaguzi wa mazoezi ya chezo cha kimwili kwa barabara na miraba ya umma, na ziara ya Ngome ya Shali na Jumba la Makumbusho la Urithi, na kuelekea Kituo cha Mawasiliano na Ujumuishaji wa Hisi, na ukaguzi wa shughuli za mpango wa michezo kwa ajili ya maendeleo (Afya yangu ndio kipaji changu) katika Kituo cha Vijana cha Siwa, na kuhudhuria semina ya kitamaduni kwa vyama mbalimbali kwa ushiriki wa vijana na wazee na viongozi na wazee wa oasis ya Siwa katika kijiji cha Olimpiki cha vikosi vya ulinzi.