Waziri wa vijana na michezo akutana na wanachama wa mamlaka ya kibunge mkoani Matroh

Wakati wa mkutano:
Dkt. Ashraf Sobhy anaelekeza kupanga uanzishaji wa klabu ya upigaji risasi na wapanda farasi hapa Matroh
baada ya kuwasili kwa ofisi kuu mkoani Matroh Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo na Jenerali Khaled Shoaib, Gavana wa Matroh walikutana na wanachama wa mamlaka ya kibunge mkoani kwa mahudhurio ya viongozi wa mashirikisho maalumu, na hivyo kabla ya kuanza mpango wa ziara yake ya Matroh, unaojumuisha taasisi kadha za vijana na michezo.
Mkutano uliojumuisha umuhimu wa uratibu na wawakilishi wa mkoa kudhamini kufikia manufaa makubwa ya rasilimali zinazopatikana mkoani, ili kuimarisha huduma zinazotolewa kwa vijana mkoani Matroh, sambamba na mipango ya uanzishaji ya wizara, pamoja na kuonesha maombi yote ya wawakilishi, na miradi ya vijana na michezo iliyotekelezwa na Wizara ya Vijana na Michezo mkoani Matroh.
Kwenye mkutano huo, Waziri huyo alisifu juhudi za wanachama wa baraza la wawakilishi na seneti inayosaidia sekta ya vijana na michezo, akisisitiza kutekeleza maombi yote ya wabunge yanayonufaisha vijana mkoani Matroh ndani ya umuhimu mkubwa unaopewa na uongozi wa kisiasa kwa mikoa yote ya mpaka.
Dkt. Ashraf Sobhy ameelekeza kupanga uanzishaji wa klabu ya upigaji risasi na wapanda farasi mkoani Matroh na inafanana na ile klabu ya upigaji risasi na wapanda farasi kwenye kata ya Wadi Al Natron mkoani Albehira.
Kwa upande wake, Jenerali Khaled Shoaib alisifu jukumu muhimu la Wizara ya Vijana na Michezo la kuandaa mipango na programu inayochangia kujenga tabia wa wamisri na kueneza maadili chanya kati ya vijana, ndani ya malengo ya mpango wa urais "bedaya inayomaanisha mwanzo" unaolenga kujenga mwanadamu wa kimisri haswa Vijana, akisifu ujali mkubwa wa Wizara ya Vijana na Michezo kutekeleza shughuli na matukio kadha mkoani Matroh, pamoja na kuzingatia miundombinu ya Vijana na Michezo.
Wawakilishi wa mkoa walisifu juhudi za ushirikiano ulizaa matunda kati ya wizara ya vijana na michezo na mkoa wa Matroh kwenye kuendeleza miundombinu, miradi na mipango iliyochangia kikubwa kuboresha hali ya maisha mkoani, na kufungua njia mpya mbele ya vijana ili kucheza michezo na kushiriki kwenye shughuli za kijamii na kiutamaduni.
Programu ya ziara ya Waziri huyo ilipangwa kujumuisha kukagua kambi ya jumuiya ya skauti ya bahari kando ya kituo cha huduma ya awali ufukweni, na kufanya kikao kwenye maktaba ya umma ya Misiri na vijana vya mkoa (wanachama wa mamlaka ya kibunge, viongozi wa klabu na vituo vya vijana, wanachama wa muundo wa kuiga wa baraza la seneti, bunge la vijana na wachipukizi, vikundi vya vijana, wahitimu wa chuo cha Nasser, wanachama wa vilabu vya kujitolea, na klabu ya uongozi wa vijana)
Pia, mpango unaojumuisha, ufunguzi wa uwanja wa wachezaji watano kwenye kituo cha vijana mkoani Matroh, kuhudhuria mechi ya soka kwenye fainali ya olimpiki ya mikoa ya mpaka, kukagua shughuli za skauti kwenye kituo cha vijana mkoani humo, kuangalia maonesho ya bidhaa za vilabu vya wasichana na wanawake, maonesho ya mipango iliyoshinda kwenye programu ya "natasharak" ya mipango ya kijamii, maonesho ya sanaa nzuri, klabu ya utamaduni, na pia mechi ya mpira wa mikono ndani ya fainali ya olimpiki ya mikoa ya mpaka kwenye Matroh, na kuonesha mradi wa kitaifa wa bingwa wa olimpiki wa judo, pia, mradi wa kitaifa alf bint alf helm (wasichana elfu ndoto elfu), na maonesho ya michezo kwa timu ya Usawa (mazoezi ya mwili).
Aidha, Mpango huo unajumuisha ukaguzi wa matukio ya programu ya yalla kamb mjini Siwa, kushiriki kwenye tamasha la kutembea, kukagua mafunzo ya usawa wa kimwili kwenye mitaa na viwanja vya umma, ziara kwa ngome ya Shali na makumbusho ya urithi, kuelekea kwa kituo cha hotuba na ushirikiano wa hisia, kukagua shughuli za mpango wa michezo kwa ajili ya maendeleo (Afya yangu ndio Kipaji changu) kwenye kituo cha vijana mjini Siwa, na kuhudhuria semina ya kuelimisha kwa mashirikisho maalumu kuhudhuriwa na vijana, masheikh, wenye hekima na viongozi wa Siwa kwenye kijiji cha olimpiki kwenye vikosi vyenye silaha.