Waziri wa Vijana na Michezo akutana na Kikosi cha 27 cha Diploma ya Usimamizi wa Michezo CIES kwa Ushirikiano na FIFA

Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alikutana na kikosi cha 27 cha programu ya Cheti cha Utaalamu katika Usimamizi wa Michezo unaotolewa na Chuo Kikuu cha Kairo kwa kushirikiana na Kituo cha Kimataifa cha Masomo/Mafunzo ya Michezo (CIES) chini ya Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA), katika makao makuu ya Wizara katika mtaa wa serikali katika mji mkuu mpya wa kiutawala.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Dkt. Omar Muhib, Mratibu Mkuu wa Diploma na FIFA, Dkt. Mohamed Kotb, Meneja wa Diploma, na viongozi kadhaa kutoka Wizara ya Vijana na Michezo.
Mwanzoni mwa mkutano, Waziri na wageni walishuhudia maonesho, ambayo yalifafanua juhudi za Wizara ya Vijana na Michezo, muundo wa shirika, kisheria na kiutekelezaji wa wizara na makoa yake katika mikoa mbalimbali, pamoja na shughuli zinazofanywa na wizara kupitia idara na sekta zake zote.
Wakati wa mkutano, pia ilifafanuliwa mwelekeo na dhana za Mkakati wa Kitaifa wa Waziri ya Vijana na Michezo, Ofa ya uwekezaji katika vituo vya vijana na vilabu, uwekezaji wa michezo kwa ujumla, utalii na shughuli za michezo, na miradi ya kitaifa kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ya ndani na kimataifa.
Katika hotuba yake, Dkt. Ashraf Sobhy alisisitiza kuwa programu ya Cheti cha Utaalamu katika Usimamizi wa Michezo ni moja ya programu muhimu zinazochangia katika kuandaa watu wenye ujuzi wa michezo kulingana na viwango vya kisasa vya kimataifa, akionesha kuwa wizara inaipa kipaumbele maalum ukuzaji wa uwezo wa kiusimamizi katika uwanja wa michezo.
Waziri wa Vijana na Michezo aliongeza kuwa programu za aina hii zinachangia katika kuandaa watu wenye ujuzi wa kusimamia taasisi za kimichezo kwa ufanisi na ujuzi, kama inavyofaa mabadiliko ya kisasa katika ulimwengu wa usimamizi wa michezo. Waziri huyo alikuwa alisisitiza kuwa Wizara ya Vijana na Michezo inasaidia mipango yote inayolenga kuendeleza michezo ya Misri, iwe kwa njia ya ushirikiano na mashirika ya kimataifa kama vile FIFA na CIES, au kupitia utekelezaji wa programu za mazoezi ya urekebishaji za ndani.
Sobhy alibainisha kuwa wizara inafanya kazi katika kuandaa mazingira kamili ya michezo, yanayojumuisha uboreshaji wa makao, kusaidia uwekezaji wa michezo, na kupanga shughuli kubwa za michezo.
Muundo wa Diploma unahusu usimamizi wa michezo, uuzaji wa michezo, ufadhili wa michezo, usimamizi wa matukio ya michezo, mawasiliano ya michezo, na sheria ya michezo, ambapo mada hutolewa na kocha wenye ujuzi wa hali ya juu katika nyanja zote za usimamizi wa michezo.
Pia, programu hutoa vikao maalum na wasemaji makuu kutoka FIFA/CIES na semina maalum kuhusu masuala yanayoibuka ikiwa ni usimamizi wa kumbukumbu, usimamizi wa mazingira magumu, ufadhili, usimamizi wa rasilimali, amani na usalama wa kimichezo katika ulimwengu wa michezo.