Waziri wa Vijana na Shirika la " Confejes " wanatoa ruzuku kwa vijana wenye miradi midogo midogo

Katika sehemu ya ushirikiano wa kimataifa kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na Shirika la Confejes, linaloshirikiana na Shirika la Kimataifa la La Francophonie, Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alitoa udhamini kadhaa kwa vijana wenye biashara ndogo ndogo. Ruzuku hizo ni sehemu ya programu ya kusaidia na kufadhili mradi, ambayo hutekelezwa kila mwaka chini ya usimamizi wa Utawala Mkuu wa Uwezeshaji Vijana kwa ushirikiano na shirika katika nchi wanachama.
Naibu Mkurugenzi wa Programu za Vijana katika tasisi ya Confejes Bw.Ibrahim Boubaker Kalousi, Mkaguzi wa Fedha wa tasisi Paul Joachim Vignino Godono na kutoka Wizara ya Vijana na Michezo Meja Jenerali Ihab Al-Basheer Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Dkt.Ashraf Elbejriemi mkuu wa sekta ya michezo na Bi. Manal Gamal wa Utawala Mkuu wa Uwezeshaji Vijana wailihudhuria Hafla ya makabidhiano hayo.
Tukio hili linakuja ndani ya mfumo wa Mpango wa Ufadhili wa Biashara Ndogo katika nchi wanachama wa tasisi, ambao unalenga kusaidia na kuwawezesha vijana kiuchumi kwa kutoa ruzuku za kifedha na kiufundi ili kuendeleza miradi yao, kuunda fursa za kazi endelevu, na kuimarisha mchango wao kwa uchumi wa ndani na wa jamii.
Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alisisitiza umuhimu wa kuwekeza katika nguvu za vijana, ambazo zinanufaisha jamii na nchi nzima. Alieleza kuwa ushirikiano wa kimkakati kati ya Wizara na tasisi ya Confejes unalenga kuwawezesha vijana kiuchumi na kukuza ujasiriamali kwa jamii.
Nchi ya Misri, iko na uongozi wa kisiasa, inaweka umuhimu mkubwa katika kutoa njia halisi kwa vijana kufanya kazi, kuzalisha, na kuvumbua.
Waziri aliongeza kuwa Wizara ya Vijana na Michezo inajitahidi kila wakati kufungua upeo mpya kwa kila kijana mwenye ndoto anayotaka kuigeuza kuwa mradi wenye mafanikio. Ruzuku hizo zinaonesha maoni ya taifa la Misri ya kujenga uchumi wa kimaendeleo ambapo vijana wanashiriki kikamilifu na ni washirika katika maendeleo na kufanya maamuzi.
Wajumbe hao wa Confejes pia wameelezea kushukuru kwao kwa ushirikiano wa karibu na Wizara ya Vijana na Michezo, na kupongeza juhudi za Misri katika kutekeleza mipango endelevu inayolenga kuwawezesha vijana kiuchumi na kukuza ubunifu na ujasiriamali ndani ya dira iliyo wazi ya kujenga kizazi chenye tija na ushawishi katika jamii yake.
Ikumbukwe kuwa Taasisi ya Confejes, iliyoanzishwa mwaka wa 1969, ni tawi la Shirika la Kimataifa la Francophonie. Inafanya kazi kusaidia serikali za nchi wanachama katika kuunda na kutekeleza sera na mikakati inayohusiana na vijana na michezo. Kupitia programu zake mbalimbali, inachangia kufadhili miradi midogomidogo na kusaidia maendeleo ya vijana katika nchi za Kifaransa.