CAF yamtuza Rais El Sisi Tuzo ya Kifahari kwa Mafanikio Bora


Kwa niaba ya Mhe. Rais El-Sisi, Rais wa Jamhuri, Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo,  amepokea tuzo iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa Mhe.Rais , wakati wa sherehe ya utoaji wa Tuzo za CAF za mwaka 2024.


Waziri huyo alionesha heshima yake kubwa ya kupokea tuzo ya kifahari kwa mafanikio bora kwa mwaka 2024 kwa niaba ya Mheshimiwa Rais. Tuzo hiyo ni tuzo ya juu kabisa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kwa kutambua juhudi bora na mchango mkubwa katika maendeleo na ukuaji wa Soka nchini Misri na Barani Afrika.


Katika sherehe hiyo, Waziri huyo alitoa shukrani za Rais wa Shirikisho la Soka Afrika kwa kumpa tuzo hiyo.


Pia klabu ya Al-Ahly ilikuwa imeshinda tuzo ya Klabu Bora ndani Afrika, ambayo ilipokelewa na Mohamed Al-Ghazawi, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.

Inayohusiana na mada hii: