البحث

Waziri wa Vijana na Michezo ashiriki katika sherehe za "Siku ya Yatima" katika bustani la Al-Azhar

2025/04/12


Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alishiriki katika sherehe ya "Siku ya Yatima" iliyoandaliwa na mkoa wa Cairo katika  bustani la Al-Azhar. Sherehe hiyo iliyoshirikiwa na takriban watoto 250, ilihudhuriwa na mawaziri na viongozi kadhaa.


Dkt. Ibrahim Saber, Gavana wa Cairo, Dkt. Manal Awad, Waziri wa Maendeleo ya Mitaa, Dkt. Osama Al-Azhari, Waziri wa Wakfu, na Bw. Mohamed Gebran, Waziri wa Kazi walihadhiriwa sherehe hiyo, katika mazingira ya kiutu, na ya burudani yenye lengo la kusaidia watoto na kuthamini jukumu la familia mbadala.


Matukio hayo yalijumuisha chakula cha mchana, maonesho ya sanaa, warsha za kuchora, mashindano, na usambazaji wa zawadi, nguo na vinyago kwa watoto. Idadi ya akina mama  pia walituzwa, katika ishara ya kibinadamu inayoakisi kujitolea kwa serikali kusaidia makundi yaliyo hatarini.


Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alisisitiza kwamba ushiriki wa wizara katika sherehe hiyo unatokana na jukumu lake la kijamii na kibinadamu, na dhamira yake ya kuwajumuisha watoto yatima katika shughuli za burudani na kiutamaduni.


Sobhy alieleza kuwa matunzo ya serikali kwa watoto wake katika kundi hili; Inaonyesha maagizo ya uongozi wa kisiasa kujenga jamii jumuishi na inayounga mkono makundi yake yote.