Mhandisi Abdel Aziz Salem, Mkuu wa Kwanza wa Shirikisho la Afrika la Soka


Mhandisi. Abdel Aziz, alirudi Misri pamoja na ndoto na mafanikio yake ili kuteuliwa katika Wizara ya Kilimo kwa muda wa miaka miwili, baadaye alihamia kufanya kazi katika Wizara ya Maarifa, lakini miaka miwili baadaye aliamua kurufi kwa Wizara ya Kilimo ili kufanya kazi katika Maslahi ya Mali ya Kifalme
Mhandisi. Salem, alipandisha cheo kama wakala msaidizi hadi alipostaafu, na mnamo kipindi hicho hicho, Mhandisi. Salem, alichaguliwa kuwa Naibu katika Baraza la Bunge kwa vipindi viwili.
Wakati wa Mapinduzi ya kimisri yalipoanza mnamo Julai 23,1952 jina la mhandisi Abd El Aziz Abd Allah Salem lilirudi mara tena, alipoteuliwa waziri wa mambo ya ndani na vijijini katika Wizara ya Ali Maher Basha, hiyo ilikuwa kabla ya kuanzishwa kwa Wizara ya Kilimo, iliyoanzishwa na mapinduzi 1952, kisha akawa Waziri wa Vijijini katika serikali ya kwanza ya Misri baada ya mapinduzi ya Julai 1952,kisha akawa Waziri wa Kilimo Katika serikali ya kwanza mnamo Septemba 7 ya mwaka huo, Ikiongozwa na Jenerali Mohammed Nageeb
Mnamo Novemba 24, 1952, Mhandisi. Salem alihudhuria tafrija katika Klabu ya Maafisa wa Jeshi ili kuzungumzia Sheria ya Marekebisho ya Kilimo na athari zake kwa maisha ya Wamisri, akisisitiza kwamba uzalishaji wa kilimo hautaathiriwa na ugawaji wa ardhi kwa wakulima wadogo.
Wakati wa vikao hivi vitatu, Mhandisi Abdel Aziz Abdullah Salem alikuwa na uangalifu ya kuhudhuria mikutano ya Baraza Kuu la Shirikisho la Kimataifa huko Zurich, Uswizi. Na wakati wa mikutano ya FIFA mnamo 1954, Mhandisi Salem alidai haki ya Misri ya kuwa mjumbe wa Ofisi ya Kiufundi ya Shirikisho la Kimataifa na mara ya kwanza, ombi lake lilikataliwa vikali.
Mhandisi Abdel Aziz Salem alitishia kujiondoa,na tayari aliondoka kutoka kwa mkutano ila katibu wa FIFA ameshughulikia suala hilo na amwombe Mhandisi Abdel Aziz Salem arudi kwenye mkutano na kusikiliza mahitaji yake,na mara tu baada ya kurudi tena alipewa nafasi ya kuzungumza,na alizungumza mbele ya hadhira kwa Kiingereza kwa ufasaha uliowashangaza washiriki,na kubadilisha taswira ya kiakili ya hadhira kuhusu mmisri wa zamani mwenye kofia nyekundu, na mwishoni mwa mkutano huo,Misri ilikubaliwa katika ofisi ya kiufundi ya Shirikisho la Kimataifa.
Mnamo Juni 1956,na pembezoni mwa kufanyika mikutano ya FIFA Congress katika mji mkuu wa Ureno huko Lisbon; Mhandisi Abdel Aziz Salem, Mkuu wa Shirikisho la Soka la Misri, Mohamed Latif, Youssef Mohamed kutoka Sudan, Abdel Rehim shadad,Badawi Mohamed na Abdel Halim Mohamed,na mwaafrika kusini Willam Phill wamekutana Kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuanzisha Shirikisho la Soka la Afrika(Baraza linalosimamia Soka Barani Afrika) kwa msaada wa Rais Gamal Abdel Nasser.
Manamo Februari 8, 1957.wawakilishi wa Misri,Sudan,na Afrika kusini walikutana na wawakilishi wa Shirikisho la Ethiopia walijiunga nao katika Hoteli ya Grand katika mji mkuu wa Sudan huko Khartoum ,na rasimu ya sheria iliwekwa na kujadili upangaji wa toleo la kwanza la Kombe la Mataifa ya Afrika.
Na baada ya kuidhinisha vifungu vya mfumo wa kimsingi, Mmisri Abdulaziz Abdullah Salem alichguliwa kuwa Mkuu kwa wingi wa kura, kwa hivyo akawa Mkuu wa kwanza katika historia ya Shirikisho hilo.
Mnamo siku ya kumi ya mwezi huo huo wa Februari, na baada ya mkutano wa kwanza wa jumuiya wa Shirikisho hilo, Mji mkuu wa Sudan ulishuhudia mwanzo wa Kombe la Mataifa ya Afrika, na hiyo kwa matakwa ya Dkt. Abdulhalim Mohammed, Mkuu wa Shirikisho la Sudan kwa Mpira wa Miguu, na kwa heshima kwa jukumu lake katika uungaji wa mkono kwa mhandisi Salem na juhudi zake kubwa katika kuanzisha Shirikisho la Afrika. Na kwa wingi wa kura mashindano ya kwanza ya Kombe yalipewa jina la mhandisi Abdulaziz Salem kwa heshima kwa juhudi zake kwa kuwa mmoja wa wakuu wa Mpira wa Miguu wa kiafrika na mwenye sababu ya kwanza katika kuujitokeza kwenye uwanja wa kimataifa. Mhandisi Abdulaziz Salem alinunua Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mali yake kutoka Khan El-Khalili nchini Misri, na linafanana na kombe la Ligi ya Mabingwa ya Uingereza .
Na hiyo ilikuwa mwanzo wa safari yenye furaha,uhai na nyakati nyingi zisizoweza kusahaulika hadi leo na hatua zinazoelekea kufafanua sura na sifa za Soka la Afrika.