Klabu ya Al- Masry

Ilianzishwa baada ya mapinduzi ya 1919 ili kupambana na Wakoloni

Klabu ya Almasry ilianzishwa mnamo tarehe Machi 18, mwaka 1920, wakati wa uzalendo wa kimisri unaokataa ukoloni wa Uingereza baada ya mapinduzi ya 1919 , ikaitwa jina hilo kwani ilianzishwa mabegani mwa wamisri kati ya idadi ya klabu nyingi mkoani Portsaid zilizohusika kwa ajili ya wakimbizi wa wazungu .
Klabu ya Almasry huko Portsaid inazingatiwa ni
klabu ya kwanza ya kimisri inayokusanya wamisri katika mapambano dhidi klabu za
kizungu, inawakilisha sura mpya ya kupambana na kuwepo kwa kizungu na
kuthibitisha utambulisho wa uzalendo katika nyanja zote miongoni mwao ni mchezo
na haswa mpira wa miguu.
Klabu hiyo ilichukua jina lake kutoka kwa wimbo wa
" Qum ya Masri " (Simama, ewe mmisri) wa kizalendo kwa msanii wa
Sayed Darwesh , msanii wa watu , pia ilichukua sare zake kutoka kwa
bendera ya kimisri ya kijani wakati huo .